MABOSI wa Yanga SC inaelezwa kuwa wamedhamiria kulipa kisasi baada ya watani zao wa jadi kuanza kuwatikisa kwenye suala la usajili kuelekea msimu wa 2025/26.
Kete ya kwanza kwa Yanga SC kushinda ilikuwa kuinasa saini ya Balla Conte ambaye tayari ametambulishwa Yanga SC kwa kandarasi ya miaka miwili.
Mchezaji huyo inatajwa kuwa Simba SC walikuwa kwenye rada za kuiwania saini yake pia wakapishana na watani zao wa jadi.
Rasmi Julai 18 Yanga SC walimtambulisha Balla kuwa mchezaji wao mpya kuelekea msimu wa 2025/26.
Inaelezwa kuwa kuna beki mwingine atachomolewa ndani ya kikosi cha Simba SC ambaye ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr na atasaini kandarasi ya miaka miwili.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC kuhusu usajili alibainisha kuwa watafanya kazi kubwa kusajili wachezaji ambao watakuwa na ubora kitaifa na kimataifa.
“Tutafanya usajili mzuri na makini kwa ajili ya wachezaji ambao watakuwa imara kitaifa na kimataifa. Tunaamini kazi haitakuwa nyepesi ila tupo imara.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.