WINGA wa Simba SC, Ellie Mpanzu anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wataondoka ndani ya kikosi cha Simba SC kutokana na ofa ambazo zipo mezani.
Inaelezwa kuwa Klabu ya RS Berkane Waarabu wa Morocco wamekubali uwezo wa nyota huyo katika anga la kitaifa na kimataifa jambo linalotajwa kuwaleta Tanzania kufanya mazungumzo na Simba SC.
Mpanzu ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba SC kwenye dirisha dogo ambapo aliibuka hapo akitokea Klabu ya AJ Vainqueur. Timu hiyo inacheza ligi ya Epfkin (Ligi ya tatu Congo).
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa kwa wanaomtaka mchezaji huyo lazima wawasiliane na Simba SC ambao ni wamiliki halali wa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo aliwahi kucheza AS Vita ya Dr Congo ambayo ilimpa utambulisho. Wengi wanatambua kwamba anatokea kwenye timu hiyo jambo ambalo limezua gumzo. Tetesi zinaeleza kuwa watani zao wa jadi Yanga SC nao wanaiwinda saini ya winga huyo kama ilivyo kwa RS Berkane.
“Mpanzu alisaini mkataba wa miaka miwili kwa sasa bado mwaka mmoja na miezi mingine mingi kwelikweli. Kama wanamuhitaji Mpanzu wanapaswa kufuata utaratibu na bei yake sio ndogo.”
Simba SC bado ina mkataba na Ellie Mpanzu ambaye ndani ya ligi kafunga mabao manne. Mbali na kufunga mabao hayo katengeneza jumla ya pasi tatu za mabao. Rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 17 akitumia dakika 1,239
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.