Klabu ya Simba imeanza rasmi mpango wa kusuka upya kikosi chake kwa msimu ujao kwa kufanya mabadiliko makubwa, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kocha Mkuu Fadlu Davids na uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha wanarejea kwenye ubora wa juu kitaifa na kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja kutoka ndani ya klabu hiyo, tayari wachezaji sita wa kigeni wametajwa kuwa sehemu ya wale wanaoachwa katika kikosi cha wekundu wa Msimbazi: Orodha ya Wachezaji Wanaotarajiwa Kuachwa:
Valentino Nouma
Augustine Okejepha
Che Marlone Fondoh
Christian Leonel Ateba
Fabrice Ngoma
Deborah Fernandes Mavambo