CÉLESTIN ECUA AJIUNGA NA YANGA SC KUTOKA ZOMAN FC

Uongozi wa mchezaji wa kimataifa Célestin Ecua umetangaza rasmi kuwa kiungo huyo sasa ni mchezaji halali wa klabu ya Yanga SC ya Tanzania, akitokea Zoman FC.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ecua alisaini mkataba na Yanga takriban wiki tatu zilizopita, kama ilivyoripotiwa awali, na sasa mipango yote imekamilika rasmi.

“Ni kweli. Célestin alisaini mkataba na Yanga wiki tatu zilizopita. Tumejiridhisha na kila kitu, na tunathibitisha rasmi kuwa ataitumikia klabu hiyo kuanzia msimu ujao,” imeeleza taarifa kutoka kwa wawakilishi wake.

Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Tanzania mwishoni mwa wiki hii ili kuanza rasmi maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa ambayo Yanga watashiriki.