KAIZER CHIEFS KUVUNJA BENKI KUIPATA SAINI YA AHOUA

KIUNGO mshambualiaji wa Simba SC Jean Ahoua raia wa Ivory Coast mkataba wake umesalia mwaka mmoja kuwa ndani ya kikosi cha Simba SC.

Alitambulishwa Julai 3 2024 kwa kandarasi ya miaka miwili yeye ni raia wa Ivory Coast. Amekuwa na msimu bora licha ya Simba SC kupishana na mataji yote iliyokuwa inayasaka.

Ikiwa Kaizer Chiefs watahitaji huduma yake wanapaswa kuvunja mkataba wa kiungo huyo mwenye mabao 16 na pasi 9 za mabao.

Kahusika kwenye mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC. Nyota huyo amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Ikiwa mabosi wa Kaizer Chiefs watakuwa wanahitaji saini ya kiungo huyo wanapaswa kuvunja benki kwa sasa kwa kuwa bado ana mkataba na Simba SC.

Kwa mujibu wa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa wachezaji ambao wanahitajika Simba SC wapo hivyo utaratibu ukifuatwa watauzwa.

“Kuna wachezaji ambao wanahitajika na timu nyingine hasa ukizingatia kwamba Simba SC ina wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa. Ikiwa utaratibu utafuatwa basi tutawauza kama tutakuwa tuna mpango wakumuweka sokoni.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.