VIGOGO 8 WATINGA ROBO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LA VILABU NCHINI MAREKANI

Michuano ya kihistoria ya Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA inayoendelea nchini Marekani imeingia katika hatua ya robo fainali huku timu nane bora zikibainika baada ya mechi kali na ushindani wa kiwango cha juu.

Timu hizo, ambazo zimeonyesha ubora wa hali ya juu kutoka mabara mbalimbali, sasa zitachuana kuwania tiketi ya nusu fainali katika toleo hili la kwanza kabisa la Kombe la Dunia la Klabu likiwa na mfumo wa timu 32.
πŸ‡©πŸ‡ͺ Bayern Munich
πŸ‡©πŸ‡ͺ Borussia Dortmund
πŸ‡§πŸ‡· Palmeiras
πŸ‡§πŸ‡· Fluminense
🏴 Chelsea
πŸ‡«πŸ‡· Paris Saint-Germain (PSG)
πŸ‡ͺπŸ‡Έ Real Madrid
πŸ‡ΈπŸ‡¦ Al Hilal

Ni michuano ya kihistoria ikiwa ni mara ya kwanza kuhusisha mfumo mpya wa timu 32, huku vikosi hivi vikitajwa kuwa miongoni mwa vigogo wa soka duniani. Vita ya ubingwa sasa inazidi kupamba moto!