SIMBA SC inayonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids inaelezwa kuwa kwenye mpango wa kuachana na mastaa wake zaidi ya watano kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
Simba SC imemaliza ligi ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo. Pointi 78 baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700. Safu ya ushambuliaji imefunga mabao 69 ikiwa namba mbili kwa timu ambazo zimefunga mabao mengi.
Kwenye orodha ya mastaa ambao wataondoka Simba SC, Fabrince Ngoma huyu ameshawashukuru Simba SC hivyo wengine wanafuata.
Ngoma alisajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili hivyo mazungumzo kwenye kuongeza mkataba wake pengine hayajafikia maafikiano mazuri.Wachezaji wengine ambao wanatajwa kuwa kwenye mpango wa kusepa ndani ya Simba SC ni Joshua Mutale.
Mutale hajawa kwenye kiwango bora licha ya kufunga bao moja kwenye mchezo wa fainali dhidi ya RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Mbali na Mutale inaelezwa kuwa Ayoub Lakred ambaye ni kipa wa Simba SC naye hatakuwa kwenye kikosi hicho msimu ujao.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.