RAIS MWINYI AWAPONGEZA YANGA SC

MAKOMBE matano ambayo Yanga SC imeyatwaa msimu wa 2024/25 yamefika Ikulu ya Zanzibar na zawadi wakakakabidhiwa Yanga SC ikiwa ni sehemu ya kutambua mafanikio ambayo wamefikia.

Rais wa Klabu ya Yanga SC, Iniinia Hersi Said alimkabidhi makombe hayo matano Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi ambaye aliwapongeza Yanga SC kwa mafanikio hayo.

Hayo yote yalifanyika katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Zanzibar Juni 30 na walipotoka huko Yanga SC walifanya paredi la Kihistoria Dar.

Mataji hayo matano ambayo Yanga SC imetwaa ni Kombe Toyota Cup hili walichukua nchini Afrika Kusini walipoalikwa katika maandalizi ya msimu wa 2024/25, Ngao ya Jamii, Muungano Cup, Ligi Kuu Bara ya NBC na CRDB Federation Cup.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi , Mawasiliano, Ikulu Zanzibar, Ragey Mohamed Juni 30 2025 ilieleza kuwa Rais Mwinyi aliwapa Yanga SC zawadi ya shilingi milioni 100 kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa ambayo wamepata Yanga SC, 2024/25.

Rais Mwinyi ameishukuru Yanga SC kwa kuendelea kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya Tanzania kupitia kampeni ya Visit Zanzibar na ameeleza kuwa klabu hiyo kuchagua baadhi ya mechi kucheza Zanzibar kunachangia kukuza uchumi na sekta ya utalii kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni na Wananchi kunufaika na fursa mbalimbali.

Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi alimkabidhi Rais Mwinyi medali maalumu ya michuano ya CRDB pamoja na jezi ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, (NBC Premier League).

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.