MOHAMED Hussen Zimbwe Jr ameweka wazi kuwa watarejea msimu ujao wa 2025/26 wakiwa imara kwenye kupambania mataji ambayo watashiriki kwenye mechi za ushindani msimu mpya.
Ipo wazi kwamba msimu wa 2024/25 Simba SC imepishana na mataji yote iliyokuwa ikipambania. Kombe la CRDB Federation iligotea hatua ya nusu fainali ikiodolewa na Singida Black Stars iliyopoteza fainali kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga SC.
Katik ligi iligotea nafasi ya pili pointi 78 baada ya mechi 30 na bingwa ni Yanga SC mwenye pointi 82 akitwaa taji la 31 la ligi kwa mujibu wa rekodi.
Zimbwe amesema kuwa walijipanga kupata mataji kwenye msimu mpya na mwisho wameambulia patupu hivyo watajipanga kwa wakati ujao.
“Tulijapanga kupata makombe kwenye msimu mpya na mwisho hatujapata kitu chochote. Kwa kilichotokea sina cha kusema ila tutajipanga kwa wakati ujao kuwa imara zaidi.”
Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ilitinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika ikagotea nafasi ya pili kwa kupoteza fainali jumla ya mabao 3-1 dhidi ya RS Berkane ya Morocco.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.