BENCHI la ufundi la Simba SC limebainisha kuwa mchezo wao dhidi ya Singida Black Stars wanatambua utakuwa ni mgumu kutokana na uimara wa wapinzani wao ila wapo tayari kupambana kupata pointi tatu muhimu.
Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids imetoka kucheza mechi mbili za fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane ikigotea kuwa mshindi wa pili.
RS Berkane ni mabingwa wakipata ushindi wa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Simba SC ya Tanzania kwa kuwa mchezo wa kwanza Mei 17 2025 ilikuwa RS Berkane 2-0 Simba SC na mchezo wa pili Mei 25 2025 ilikuwa Simba SC 1-1 RS Berkane.
Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amesema wanatambua uimara wa wapinzani wao jambo linalowafanya waingie kwa tahadhari.
“Ni mpinzani mwenye timu imara sio wakubeza hasa ukizingatia matokeo ambayo anapata uwanjani, tumetoka kucheza mechi ngumu hilo lipo wazi lakini ratiba tulikuwa tunaijua hivyo tupo tayari kwa ajili ya pointi tatu.”
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 28 2025 Uwanja wa KMC Complex saa 10:00 jioni ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Timu hizo zimekutana mara nane katika michuano yote na Singida haijawahi kupata ushindi zaidi ya kutoa sare mara moja huku ikifungwa michezo saba .
Singida itaingia uwanjani katika mchezo huo kwa lengo moja pekee la kutaka kuvunja rekodi ambayo wanayo Simba ya kutoifunga.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.