BEKI WA KAZI SIMBA SC KAMILI KUWAKABILI RS BERKANE MEI 25 2025

SIMBA SC wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika, Mei 25 2025 watakuwa na kazi nzito mbele ya RS Berkane kwenye mchezo wa fainali ya pili la Kombe la Shirikisho Afrika huku beki wao akiwa kwenye asilimia kubwa kurejea uwanjani.

 Jina lake ni Abdulrazack Hamza, yupo kwenye orodha ya wachezaji ambao wanapewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza mara baada ya kukwama kukamilisha dakika 90 dhidi ya RS Berkane kwenye mchezo uliopita ugenini alipopata maumivu.

Ipo wazi kwamba Mei 17 2025, Hamza alipata maumivu dakika ya 21 kwenye mchezo huo na nafasi yake ilichukuliwa na beki wa kazi Che Malone aliyekamilisha dakika zilizobaki kwenye mchezo huo ugenini.

Simba SC kwa sasa ipo Zanzibar kwa maandalizi ya mchezo wa fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Hamza anafanya mazoezi ya nguvu pamoja na wachezaji wenzake katika kujiandaa na mchezo wa fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo, Simba inatarajiwa kuvaana dhidi ya Berkane saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar ambao wanahitaji ushindi wa 3-0 wabebe taji hilo kwa kuwa walipoteza mchezi wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0.

Taarifa zinaeleza kuwa Hamza amepona majeraha yake aliyoyapata katika mchezo wa awali na kushindwa kuendelea katika kipindi cha kwanza, beki huyo amepona ana asilimia mia moja ya kucheza pambano hilo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.