SIMBA SC wamebainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo wa pili wa fainali dhidi ya RS Berkane licha yakupoteza kwenye mchezo wa fainali ya kwanza wakiwa nchini Morocco.
Ikumbukwe kwamba Mei 17 2025 kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya kwanza baada ya dakika 90 ubao ulisoma RS Berkane 2-0 Simba SC, mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Mei 25 2025 Jumapili, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
RS Berkane wametanguliza mguu mmoja kwenye hesabu za kutwaa taji hilo kutokana na ushindi ambao waliupata wakiwa nyumbani kwa mabao mawili waliyofunga kupitia kwa Mamadou Camara dakika ya 8 na Ousama Lamlioui dakika ya 15.
Beki wa Simba SC, Shomari Kapombe ambaye alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa ugenini na alifanya kazi kubwa katika kutimiza majukumu yake eneo la ulinzi ambalo lilikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na safu ya ushambuliaji ya RS Berkane kuwa na kasi kwenye kutafuta matokeo chanya.
“Hatujapata matokeo mazuri ugenini hilo lipo wazi ila tupo tayari kuelekea kwenye mchezo wetu wa pili tukiwa nyumbani, kikubwa ni kupata matokeo mazuri hilo linawezekana na wachezaji tupo tayari.”
Simba ili itwae taji la Kombe la Shirikisho Afrika kwenye mchezo wa nyumbani unaotarajiwa kuchezwa Mei 25 lazima wapate ushindi wa mabao 3 na wapambane safu ya ulinzi isiruhusu bao.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.