CAF YAJIRIDHISHA NA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA, SIMBA YAPATA MATUMAINI MAPYA KWA FAINALI YA CAFCC

Taarifa za kuaminika ni kuwa maafisa wa CAF wameeleza kuwa wamejiridhisha uwanja wa Benjamin Mkapa upo vizuri kwa michuano ya CHAN 2025 mwezi August ( Kenya )

Pia TFF na Simba SC imeomba review ya kuchezea uwanja huo fainali ya CAFCC baada ya ukaguzi huo wa michuano ya CHAN na CAF wamekubali review hiyo na wanalifanyia kazi haraka

Maafisa wa CAF wamejiridhisha kuwa eneo la kuchezea ( pitch ) , maeneo ya viti hadi katika vyoo kuna maboresho mazuri sana na hasa katika eneo la kuchezea ambapo mvua ilinyesha lakini hali ilikuwa vizuri sana na mpaka sasa matumaini ya Simba SC kucheza dimba la Mkapa yameanza kurudi kwa kasi baada ya ukaguzi wa leo.