SIMBA SC YASUBIRI TAMKO RASMI LA CAF KUHUSU UWANJA WA FAINALI YA CAFCC DHIDI YA BERKANE

Baada ya taarifa nyingi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu CAF kupitia barua yao ya kuwaambia TFF na Simba SC kuwa mchezo wa Fainali ya Pili ya CAFCC kati ya Simba dhidi ya Berkane upigwe New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Timu ya Simba SC, imetoa Taarifa rasmi kuhusu uwanja wa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, na kusema kwamba taarifa ya uwanja utakaotumika itatolewa baada ya mchezo wa awali utakaochezwa Jumamosi Mei 17, 2025.

Aidha, kwa taarifa kuhusu timu ya Berkane, inaelezwa tayari wameshapata sehemu ya kufikia Zanzibar kabla ya taarifa ya CAF.