KIPA namba moja wa Simba SC Moussa Camara kwenye mechi nne ambazo amekaa langoni ndani ya Mei katunguliwa mabao matatu akiruhusu bao moja kwenye mechi tatu akikwama kusepa na clean sheet katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji dakika ya 86 huku mbele ya KMC dakika ya 6 na Mashujaa dakika ya 6.
Joshua Mutale kiungo mshambuliaji ameonyesha kazi kubwa kwenye mechi zilizopita na alichaguliwa kuwa mchezaji bora mchezo dhidi ya KMC FC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex alipotoa pasi mbili za mabao zikitumiwa na Steven Mukwala katika kufunga.