MERIDIANBET YAFIKA MBEZI AFRICANA KWAAJILI YA CSR

Wababe wa ubashiri Meridianbet kama ilivyo kawaida kwao jamii ndio kila kitu kwako, hivo siku ya leo waliamua kufika Mbezi Africana pale Kituoni na kufanya zoezi la usafi.

Katika hatua ya kipekee ya kuhimiza uwajibikaji wa kijamii na kizalendo miongoni mwa vijana, kampuni ya michezo ya kubashiri ya Meridianbet ilikuja na Slogan ya  “Vijana na Mazingira Yao”, iliyoanzia kwa kishindo katika Stendi ya Africana.

Meridianbet iliandaa siku ya usafi ikishirikiana na Diwani wa Kata hiyo ya Mbezi Mheshimiwa Anna Lukindo, ofisi yake pamoja na wananchi wa eneo hilo huku lengo likiwa ni kuhakikisha Stendi hiyo inakuwa katika mazingira safi.

Meneja Mahusiano wa Meridianbet Nancy Ingram alieleza: “Hatutaki tu kuja kufanya usafi, tunataka kubadilisha fikra. Tumeamua kuanza na vijana kwa sababu wao ndiyo taifa la leo. Tukiwafikia mapema, tunalinda kesho ya miji yetu.”

Zoezi hili limehusisha usafishaji wa mazingira ya stendi, ukusanyaji wa taka na utoaji wa vifaa maalum vya usafi kama mifuko, glovu, na maji kwa washiriki, huku likilenga kuhamasisha usafi wa mazingira na mshikamano kati ya sekta binafsi, uongozi wa eneo, na jamii.

Mpango wa Kimataifa wa Usafi – Ushirikiano wa Tanzania na Serbia

Zoezi hili limefanyika kwa wakati mmoja na shughuli nyingine kama hiyo nchini Serbia, ambako Timu ya CSR ya Meridianbet Serbia imefanya usafi katika hifadhi ya Fruška Gora, sambamba na udhamini wa mbio za EPIC MTB.

Pia leo hii unaweza ukatusua kijanja na Meridianbet kwani mechi kibao zipo uwanjani .Suka jamvi lako la ushindi leo na ubashiri hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.

Kwa kufanya zoezi hili kwa pamoja, Meridianbet Tanzania imeungana rasmi na timu ya kimataifa ya Meridianbet katika kutekeleza mpango wa Usafi wa Kimataifa, ukiwa ni sehemu ya dhamira ya kampuni ya kulinda mazingira na kuchangia maendeleo endelevu katika maeneo yote tunayofanya kazi.

Kupitia kampeni hii, Meridianbet inatoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kuhifadhi mazingira na kuendeleza ushirikiano kati ya mashirika, viongozi wa serikali, na wananchi kwa

Pamoja na usafi, Meridianbet pia ilitoa mafunzo mafupi juu ya athari za uchafu kwa afya na uchumi wa jamii, na kuanzisha mtandao wa vijana wa kujitolea kusimamia usafi wa kila wiki  hatua ambayo imepokelewa kwa hamasa kubwa.

Kwa Meridianbet, hii si kampeni ya siku moja  ni mwamko mpya wa kuwasha fikra na moyo wa uwajibikaji wa kijamii. Huu ni mfano mwingine wa jinsi kampuni binafsi inaweza kuwa daraja la maendeleo na mabadiliko chanya ya jamii.