Paris Saint-Germain (PSG) wamefuzu kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kuwatoa Arsenal kwa jumla ya mabao 3-1 katika hatua ya nusu fainali. PSG walishinda mechi ya kwanza 1-0 ugenini, kisha wakamaliza kazi kwa ushindi wa 2-1 nyumbani kwenye Parc des Princes.
PSG sasa watakutana na Inter Milan katika fainali itakayofanyika Jumamosi, Mei 31, 2025, kwenye Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani. Mchezo utaanza saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).
Hii itakuwa fainali ya pili kwa PSG katika kipindi cha miaka mitano, na ya kwanza tangu kuondoka kwa Kylian Mbappé. Kwa upande wa Inter Milan, hii ni fainali yao ya saba ya UCL, wakitafuta taji lao la nne la Ulaya.