PAMBA JIJI KAMILI KUIKABILI SIMBA SC

Fred Felix Kocha Mkuu wa Pamba Jiji ameweka wazi kuwa wanatambua ugumu wa mchezo wao dhidi ya Simba SC ila wana imani kuwa hawatashuka daraja.

Ni mechi 26 imeshuka uwanjani Pamba Jiji ina pointi 27 ikiwa nafasi ya 13 katika msimamo ambayo ni nafasi yakucheza play off ikiwa itasalia hapo mpaka mzunguko wa pili ukigota mwisho.

Mechi ambazo ilipata ushindi ni 6, sare ilikuwa kwenye mechi 9 na mechi 11 ilipoteza ndani ya msimu huku safu ya ushambuliaji ikitupia mabao 17 na ukuta umeruhusu mabao 27.

Novemba 22 2024 ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba baada ya dakika 90 ulisoma Pamba Jiji 0-1 Simba SC.

Fred amesema: “Tunatambua ugumu wa mchezo lakini vijana wangu wako tayari kwa ajili ya kupambana na niwaote wasiwasi Wanamwanza na mashabiki wa Pamba Jiji kuwa timu hii haishuki daraja.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.