BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Che Malone amerejea na huenda akawa sehemu ya wachezaji watakaokuwa kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex.
Ipo wazi kwamba beki huyo alikuwa nje kwa muda mrefu baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa MzizmaDabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa mzunguko wa pili.
Ilikuwa ni Februari 24 2025 Che Malone alikwama kuendelea katika mchezo huo ambao baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Azam FC wababe hao wakigawana pointi mojamoja.
Baada ya kuwa nje kwa muda akipambania hali yake hatimaye amerejea sehemu ya mazoezi ya kikosi cha Simba SC na alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye mazoezi ya mwisho Uwanja wa KMC Complex, Mei Mosi 2025.
Mbali na kuwa sehemu ya kikosi Che Malone alipata nafasi ya kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Stellenbosch FC uliochezwa nchini Afrika Kusini ikiwa ni mkondo wa pili hatua ya nusu fainali alianzia benchi akiingia dakika ya 86 akichukua nafasi ya Ellie Mpanzu.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.