FISTON MAYELE AIPELEKA PYRAMIDS FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

FISTON Mayele mshambuliaji wa Pyramids ambaye aliwahi kucheza ndani ya Klabu ya Yanga inayoshiriki Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika alifunga mabao mawili kati ya matatu kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Orlando Pirates

Ushindi huo wa Aprili 25 2025 unaifanya Pyramids ya Misri kutinga hatua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kuiondosha Orlando Pirates ya Afrika ya Kusini kwa mabao 3-2. Kwenye nusu fainali ya kwanza wababe hawa ilikuwa 0-0 Aprili 19 2025.

Mayele alipachika mabao hayo dakika ya 45, 85 na bao jingine lilifungwa na Ramadan Sobhi dakika ya 57, yale ya Orlando yalifungwa na Relebohile Mofokeng dakika ya 41 na Mohau Nkota dakika ya 52.

Pyramids watachuana na Mamelodi Sundowns katika mchezo wa fainali baada Mamelodi kuwatoa mabingwa wa Kihistoria wa michuano hiyo Al Ahly baada ya kupata sare ya 1-1 na kupita kwa faida ya goli la ugenini.

Fainali inatarajiwa kuchezwa Mei 25 2025 nchini Afrika Kusini na mkondo wa pili itakuwa ni Julai Mosi 2025 nchini Misri.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.