CLEMENT Mzize nyota wa kikosi cha Yanga ni namba moja kwa wakali wakucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25.
Kutoka kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika, vita ni kali kwenye eneo la ushambuliaji huku kukiwa na mzawa mmoja mwenye zali lakucheka na nyavu akiwa na mabao 13.
Mzize alipachika mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate, Aprili 21 2025 ubao wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliposoma Fountain Gate 0-4 Yanga, pointi tatu zilikuwa mali ya Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 70 baada ya mechi 26 na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 68.
Prince Dube wa Yanga ambaye ni mkali kwa mabao ya vichwa ni namba mbili akitupia mabao 12 sawa na Jean Ahoua wa Simba ambaye ni mkali kwa mguu wa kulia akiwa katupia mabao yote hayo kwa mguu wa kulia.
Jonathan Sowa wa Singida Black Stars katupia mabao 11 huyu ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Singida Black Stars ambacho kipo nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi zake ni 53.
Elvis Rupia kutoka Singida Black Stars katupia mabao 10 ndani ya ligi huku Steven Mukwala wa Simba na Pacome wa Yanga hawa wametupia mabao 9 kila mmoja.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.