MILOUD Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga amepanga jeshi lake la kazi kamili kwa ajili ya kusaka pointi tatu dhidi ya Tabora United mchezo ambao una suhindani mkubwa huku mashabiki wakiwa wamejitokeza kwa wingi.
Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Novemba 7 2024 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 1-3 Tabora United hivyo mchezo wa leo Aprili 2 2025 ni kisasi kwa Yanga na kulinda rekodi kwa Tabora United.
Kikosi kinachoanza kipo namna:-Djigui Diarra, Israel Mwenda, Boka, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Prince Dube, Pacome na Clement Mzize.
Wachezaji wa akiba ni Aweso ambaye ni kipa, Nickson Kibabage, Bakari Nondo, Kibwana Shomari, Dennis Nkane, Sure Boy, Farid Mussa na Ikanga Lombo Jonathan.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.