INAELEZWA Klabu ya Simba na Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini zimepiga hodi Singida Black Stars FC, kwa ajili ya kuulizia uwezekano wa kumpata mshambuliaji Mghana Jonathan Sowah, 25.
Nyota huyo hivi karibuni alitajwa kuwepo katika mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kuipata saini yake katika msimu ujao, ambaye anatajwa hapo Singida BS anafanya kama njia ya kumwaga wino Jangwani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Singida BS, hadi hivi hakuna ofa yoyote rasmi iliyotumwa, licha ya kuanza kuulizia uwezekano wa kumpata mshambuliaji huyo mabao Saba akicheza michezo Saba.