KOCHA SIMBA AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE

FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa pongezi kubwa kwa wachezaji wake kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya TMA Stars ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Machi 11 2025 Simba ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup dhidi ya TMA Stars ilikuwa ni Uwanja wa KMC, Complex.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 3-0 TMA Stars, mabao ya Valentin Nouma dakika ya 15, Sixtus Sabilo alijifunga dakika ya 19 na Leonel Ateba alifunga bao dakika ya 75 akitumia krosi ya Kelvin Kijili ambaye alianzia benchi kwenye mchezo huo.

Fadlu amebainisha kuwa walifanya maandalizi makubwa kwa ajili ya mchezo wa Kariakoo Dabi ambao ulighairishwa Machi 8 2025 hivyo kazi nyingine ilikuwa kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya TMA Stars.

“Tulikuwa tumefanya maandalizi makubwa mchezo wetu wa Dabi ambao haukuchezwa hivyo tulikuwa na kazi nyingine kwenye maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya TMA Stars na niliwaambia wachezaji kwamba hautakuwa mchezo mwepesi ni lazima kila mchezaji awe tayari.

“Ninawapongeza kwa namna ambavyo wamejitoa na kujituma kwa ajili ya kupata matokeo mazuri hili ni muhimu hasa kwa kuwa timu imesoga hatua inayofuata.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.