TUZO ZA TFF, PRINCE DUBE NDIYE MCHEZAJI BORA MWEZI FEBRUARI

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Prince Mpumelelelo Dube amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya NBC 2924/25 akiwashinda Stephanie Aziz Ki pia wa Yanga Sc na Selemani Bwenzi wa KenGold Fc.

Pia, kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kocha wa Yanga Sc, Miloud Hamdi ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari akiwashinda Fadlu Davids na Fred Felix Minziro.

Dube alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo saba, Yanga SC ikishinda mechi sita na kutoka sare mchezo mmoja akifunga magoli matano na kuhusika kwenye magoli mengine matano.