SINGIDA BLACK STARS KUTUMIA UWANJA WA TANZANITE KWARAA BABATI MKOANI MANYARA

Klabu ya Singida Black Stars itautumia uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo mjini Babati mkoani Manyara kama uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa Kombe la Shirikisho CRDB dhidi ya KMC FC utakaochezwa Machi 13, 2024 majira ya saa 10:00 jioni.

Taarifa Machi 10, 2025 iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars imebainisha kuwa klabu hiyo itatumia uwanja huo kutokana na kufungiwa kwa uwanja wa CCM LITI ambao ulikuwa ukitumika kwa mechi za nyumbani za Wakulima hao wa Alizeti.

“Tunapenda kuwatoa hofu mashabiki wetu kuwa Uongozi wa Klabu kwa kushirikiana na wamiliki wa Uwanja wa CCM LITI na wadau wengine mkoani Singida tunaendelea na hatua za haraka za ukarabati wa uwanja ili uweze kutumika kwenye mechi zetu zinazofuata za Ligi Kuu NBC.”——imesema sehemu ya taarifa hiyo.