WABABE WA SERIE A WAKABANA KUWANIA UBINGWA

Shughuli imemalizika katika dimba la Diego Armando Maradona mjini Naples, wenyeji Napoli wametoshana nguvu na Inter Milan kwa sare ya 1-1 kwenye mechi dume kweli kweli, Inter Milan wakiwa wa kwanza kuliona lango kupitia kwa Federico Dimarco mapema dakika ya 22 kabla ya Philip Billing kusawazisha mambo jioni dakika ya 87.

Inter wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Serie A, pointi 58 baada ya mechi 27 huku Napoli wakisalia nafasi ya pili pointi 57 baada ya mechi 27.

FT: Napoli 1-1 Inter Milan
⚽ 87’ Philip Billing
⚽ 22’ Federico Dimarco