PASCAL Msindo kwa asilimia 80 aliwanyima ushindi Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Februari 24 2025 kwenye Mzizima Dabi kutokana na kutimiza majukumu yake kwa umakini asilimia 100.
Utulivu kwenye miguu yake ulikuwa ukiwavuruga mabeki wote wa Simba ambao ni watengeneza mipango namba moja kwa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Alikuwa anatokea katika matukio yote na hata wakati Mpanzu anakwenda kufunga bao la kusawazisha tayari alikuwa anakaribia kumkuta lakini spidi ya Mpanzu ikamkosesha namna kuzuia mpira ule.
Mwisho Simba 2-2 Azam FC, Zidane mchezaji bora wa mchezo akitumia pasi ya Feisal Salum kumtungua Camara.
Dakika ya 41 wakati Kapombe akiwa anaelekea ndani ya 18 na mpira kijana alislide na kucheza mpira alirudia tena dakika ya 56 akiwa kwenye ubora mkubwa na amekuwa akifanya hivyo kwenye mechi nyingi ndani ya Azam FC.
Mpole ukimuona, mcheshi kweli halafu mkorofi nje ya uwanja lakini ndani ya uwanja anapiga kazi kinomanoma. Kapombe ni imara kwenye mipira ya krosi akiwa nje ya 18 jambo ambalo lilikuwa likikwama kufanikiwa kwenye miguu ya kijana Msindo ambaye alipewa majukumu kwa ushirikiano na wachezaji wengine.