RATIBA YA LIGI KUU BARA BONGO, MBUZI TAMBO TUPU

LIGI namba nne kwa ubora inaendelea kuchanja mbunga ambapo l Februari 22 kunatarajiwa kuchezwa mechi mbili kali za kukata na shoka kwa wababe kuwa ndani ya uwanja.

Issa Liponda maarufu kama Mbuzi ambaye ni Ofisa Habari wa Fountain Gate ameweka wazi kuwa wapo tayari kusepa na pointi tatu muhimu ugenini kutokana na maandalizi ambayo wamefanya.

“Tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wetu muhimu tunatambua hautakuwa mwepesi ila tutakuwa ugenini kama tupo nyumbani, kikubwa ni pointi tatu muhimu.”

Ken Gold iliyo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 13 itawakaribisha KMC, wenye pointi 22 nafasi ya 11 itakuwa ni Uwanja wa Sokoine, Mbeya

Dodoma Jiji wenye pointi 23 baada ya kucheza mechi 19 itakuwa dhidi ya Fountain Gate, yenye pointi 22 nafasi ya 10 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.