MKALI wa pasi za mwisho Bongo ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo ni ligi namba nne kwa ubora Afrika balaa lake sio jepesi akiwa uwanjani kutokana na kasi anayoendelea nayo kiungo Feisal Salum mali ya Azam FC.
Timu hiyo kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 18 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 39 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 27.
Fei kahusika katika mabao 14 kati ya 27, akitupia jumla ya mabao manne na yote mguu wake wenye nguvu zaidi ni ule wa kulia kwa kucheka na nyavu.
Pasi yake ya 10 alitoa katika mchezo dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex dakika ya 65 kwa mguu wake wa kulia alimpa mshikaji wake Gibril Sillah ambaye kwenye mchezo huo uliochezwa Februari 6 2025 aliibuka kuwa mchezaji bora.
Fei amekuwa na zali dhidi ya KMC kwa kuwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa KMC Complex Septemba 19 2024 alitoa pasi yake ya kwanza dakika ya 19 alimpa Nado na katika mchezo huu yeye alichaguliwa kuwa mchezaji bora alitoa pasi mbili zilizoleta mabao nyingine alimpa Lusajo dakika ya 54.
Bao lake la kwanza msimu wa 2024/25 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Ken Gold ilikuwa Oktoba 25 2024 dakika ya 19 Uwanja wa Azam Complex kwa pigo la penalti.
Bao la pili aliwatungua Kagera Sugar dakika ya 55 Azam Complex kwa pigo la penalti, bao la tatu aliwatungua Singida Black Stars dakika ya 37 Azam Complex na bao la nne aliwatungua Dodoma Jiji ilikuwa Desemba Mosi 2024 kwa pigo la penalti.
Mabao matatu kafunga kwa penalti kati ya manne aliyonayo kiungo huyo ambaye ametumia mguu wa kulia kufunga mabao yote hayo ndani ya ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.