JINA lake anaitwa Wilson Nangu miongoni mwa wachezaji ambao wanavuja jasho ndani ya JKT Tanzania ambayo ipo ndani ya 10 bora.
Katika eneo ambalo JKT Tanzania haijawa imara sana ni eneo la ushambuliaji ikiwa na wastani mdogo katika kucheka na nyavu baada ya mechi 18 safu ya ushambuliaji imefunga mabao 11.
Eneo ambalo imekuwa imara ni eneo la ulinzi ikiwa ndani ya timu tano bora ambazo zimefungwa mabao machache, JKT Tanzania ni namba tano ikiwa imefungwa mabao 14 ndani ya mechi 18.
Ndani ya dakika 1,620 ni mabao 14 imefungwa ikiwa na wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 115 huku ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 147.
Ni timu ya kwanza kuambulia sare mbele ya Yanga baada ya ubao wa Meja Isamuhyo Februari 10 2025 kusoma JKT Tanzania 0-0 Yanga na mchezaji bora alikuwa ni Nangu.
Rekodi zinaonyesha kuwa Nangu aliokoa hatari zaidi ya 5 miongoni mwa hizo ilikuwa dakika ya 44, 45, 55, 68, 69, 73, 83, 90.
Alicheza faulo ya hatari dakika ya 69 ikawa chanzo kwake kuonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Ahmed Arajiga. JKT Tanzania kwenye msimamo ni nafasi ya 10 ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 18.