BENCHIKA KUTIMKIA MODERN FUTURE YA MISRI

Baada ya kuondoka JS Kabylie Januari iliyopita, kocha wa Algeria Abdelhak Benchikha yuko mbioni kutia saini ya kuifundisha klabu ya Modern Future ya Misri inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Benchikha, ambaye tayari amekuwa na uzoefu kadhaa nje ya nchi, hasa Tanzania,Morocco na Qatar, anaweza kujikuta akiwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo.

Modern Future FC ni klabu ya soka ya Misri yenye makao yake mjini Cairo ambapo ilianzishwa mwaka 2011,ikiwa ina miaka miaka 14 baada ya kuanzishwa kwake.

Klabu hiyo inakamata nafasi ya mwisho Ligi Kuu nchini Misri ikiwa na alama 7 katika michezo 12 iliyocheza. Imeshinda mchezo mmoja tu.