MCHEZAJI bora wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Isahmuyo, Wilson Nangu amesema kuwa amefurahi kupata tuzo hiyo akiwashukuru mashabiki pamoja na wachezaji kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Ikumbukwe kwamba baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Tanzania 0-0 Yanga hivyo wababe hao waligawana pointi mojamoja ndani ya dakika 90, kipindi cha kwanza zliongezwa dakika 3 na kipindi cha pili ziliongezwa dakika 6.
Ni mchezo wa kwanza kwa Yanga kuambulia sare ndani ya msimu wa 2024/25 katika mechi 18 ilizocheza ni ushindi kwenye mechi 15 na ilipoteza mechi mbili dhidi ya Azam FC na Tabora United.
Nyota huyo alikomba dakika zote 90 kila eneo la uwanja alikuwepo kuokoa hatari za Yanga huku beki Israel Mwenda akiwa miongoni mwa nyota waliokuwa wakipambana nao mara kwa mara hasa katika upande wa kupiga krosi kuelekea lango la JKT Tanzania.
“Nimefurahi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo haukuwa mchezo rahisi ulikuwa mchezo mgumu ukizingatia kwamba unakutana na timu yenye uzoefu na wachezaji wazuri hivyo tulipambana kutafuta matokeo mwisho tumepata pointi moja.”
Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 45 baada ya mechi 18 inafuatiwa na Simba nafasi ya pili na pointi 44 baada ya kucheza mechi 17.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.