Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Munich Jan-Christian Dreesen alithibitisha kwa kwamba klabu hiyo inafuatilia hali jinsi ilivyo nchini DR Congo.
Bayern imetuma wafanyikazi wawili nchini Rwanda baada ya kupokea ukosoaji kwa udhamini wao wa Visit Rwanda.
Tangu Agosti 2023, Bayern Munich imekuwa na Visit Rwanda kama mfadhili, mpango wa ofisi ya utalii ya Rwanda.
Mwishoni mwa juma lililopita, Kinshasa, iliyotahadharishwa na ombi lililozinduliwa na shabiki wa Paris Saint-Germain, ambayo ina mfadhili huyo huyo, iliitaka Bayern Munich na vilabu vingine viwili ikiwemo PSG kusitisha mawasiliano na Kigali.
Katika barua iliyotumwa kwa vilabu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo, Thérèse Wagnera alizungumzia hatia ya Rwanda katika mzozo wa DRC ambao anauona usiopingika.