SALEH JEMBE – ”PRESHA INAWASUMBUA – VIONGOZI HAWAMTAKI – WACHEZAJI WAMEFANYA KAMPENI AONDOKE?” – VIDEO

Kikosi cha Wananchi, Young Africans Sc kinachoanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu bara dhidi ya Ken Gold Fc utakaopigwa katika dimba la KMC Complex.

Beki wa kulia, Kibwana Shomari ambaye amekuwa na wakati mzuri tangu ujio wa Sead Ramovic ameanzia benchi muda mfupi tu tangu kuondoka kwa Mjerumani huyo huku nafasi yake ikichukuliwa na Israel Patrick Mwenda.

Djigui Diarra anaendelea kulinda lango akisaidiwa na Dickson Job, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ , Mwenda na Shadrack Boka huku Khalid Aucho na Mudathir wakiongoza safu ya kiungo cha kati.

Pacome Zouzoua, Stephanie Aziz, Clement Mzize na Prince Mpumelelelo Dube wanaongoza safu ya ushambuliaji.