KUNA pacha zinazotesa ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids miongoni mwa hizo ni ile ya Leonel Ateba na Shomari Kapombe kutokana na kujibu kwenye mechi za kitaifa na kimataifa.
Simba ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na pointi 43 mchezo wao ujao wa ligi ni dhidi ya Fountain Gate unaotarajiwa kuchezwa Februari 6 2025, Uwanja wa Tanzanite Kwalaa.
Ipo wazi kwamba Simba katika anga la kimataifa baada ya kucheza mechi sita hatua ya makundi ni mabao 8 safu ya ushambuliaji imefunga kinara wa utupiaji akiwa ni kiungo mshambuliaji Kibu Dennis.
Kapombe na Ateba wamekuwa na maelewano kazini kutokana na kila mmoja kufanyia kazi pasi ya mchezaji kwenye mechi ngumu ambazo zinahitaji pointi jambo ambalo limeongeza nafasi ya Simba kugotea nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 13.
Ilianza ugenini dhidi ya Bravos Januari 12 2025 dakika ya 69 wakati Simba ikiwa nyuma kwa bao moja pasi ya dhahabu kutoka kwa Kapombe ilikutana na Ateba ambaye alifunga bao la kuweka usawa wakagawana pointi mojamoja.
Bao la pili ilikuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Constantie Januari 19 2025 alianza Kibu kufunga bao la kuongoza kisha Ateba akafunga bao la pili akitumia pasi ya Kapombe ilikuwa dakika ya 79.
Nyota hawa wamekuwa na maelewano na dakika zao zenye hatari ni zile zenye 9 mwisho kwa kuwa dhidi ya Bravos ilikuwa dakika ya 69 na dhidi ya Constanine ilikuwa dakika ya 79.
Mwendelezo wa pacha hiyo ulijibu Tabora dhidi ya Tabora United ambapo Ateba kwenye mchezo huo alifunga mabao mawili na alitoa pasi moja ya bao kwa Kapombe ambaye aliandika bao la tatu la Simba.
Katika mchezo huo Ateba alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo kutokana na kuhusika kwenye mabao yote matatu na Simba ikakomba pointi tatu ugenini.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.