Wawakilishi wa Tanzania katika CAF Champions League Yanga SC, Novemba 28,2025 watakuwa na mchezo wa pili hatua ya makundi dhidi ya JS Kabylie.
Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Hocine Ait Ahmed Ijumaa kwa wababe hao kutoka kundi B kukutana uwanjani.
Kuna orodha ya nyota ambao wataukosa mchezo huo dhidi ya Waarabu wa Algelia kutokana na sababu mbalimbali.
Beki Kibwana Shomari, Dennis Nkane, Sure Boy, Abdulnasir maarufu kama Casemiro, Clement Mzize ambaye ni mshambuliaji, Farid Mussa, Nizar Othman Abubakar.
Yanga SC imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco katika mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.