Live CAF Champions’ League Group Stage
Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat
Uwanja wa New Amaan Complex
Novemba 22,2025
Goooal
Dakika ya 58 Prince Dube anafunga goal la kuongoza akitumia pasi ya maelekezo ya Mudathir Yahya
Kadi ya njano
Mlind mlango wa AS FAR Rabat anaonyeshwa kadi ya njano
Mabadiliko
Ecua anatoka dakika ya 56 anampisha Edmund John
Dakika ya 55 mchezo unasimama kwa muda kupisha huduma ya kwanza kwa mlinda mlango wa AS FAR Rabat
Dakika ya 53 Diarra anaokoa hatari
Dakika ya 51 mlinda mlango wa AS Far Rabat anaokoa hatari kutoka kwa kiungo Ecua Celestin
Dakika ya 50 Djigui Diarra anatoka kwenye eneo lake la 18 anaokoa hatari
Dakika ya 49 Maxi anapiga pasi mpenyezo inaokolewa na FAR Rabat
Dakika ya 45 Mudathir anacheza faulo
Kipindi cha pili
AS Far Rabat wamefanya mabadiliko kwa wachezaji wawili
Khaba ameingia kuchukua nafasi ya Slim, Khalid ametoka pia kwa AS Far Rabat
HT: Yanga SC 0-0 AS Far Rabat
Zimeongezwa dakika 3
Dakika ya 45 Zimbwe Jr anapiga faulo inaokolewa na mlinda mlango Tagnaouti
Dakika 43 Bacca anachezewa faulo na Al Fahli
Dakika ya 40 Hrimat anacheza faulo kwa Mudathir Yahya
Dakika ya 40 Ecua amecheza faulo kwa nyota wa AS Far Rabat, Carneiro
Dakika ya 36 AS Far Rabat wanafanya jaribio linakwenda nje ya lango
Dakika ya 36, Mwenda anaokoa hatari kwa kutoa mpira nje ya uwanja
Dakika ya 34 Zimbwe Jr anapiga pasi kwa Bacca
Baada ya matibabu kwa mchezaji mpira unaendelea
Mpira umesimama kwa muda
Kadi ya njano dakika ya 31
Dakika ya 31 Maxi Nzengeli anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Hammoudan
Dakika ya 30 Yanga SC wanaanzisha kona fupi inaokolewa
Dakika ya 30 mlinda mlango wa AS Far Rabat anaokoa hatari kwa pigo la Maxi Nzengeli
Dakika ya 24 Mudathir Yahya anakutwa kwenye mtego wa kuotea
Dakika ya 6, Dube anafanya jaribio akiwa ndani ya 18 inaokolewa
Dakika ya kwanza Pacome anapiga kona haileti matunda
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.