Clement Mzize ametwaa tuzo CAF ya goli bora, imerudi nyumbani

CLEMENT Mzize mshambuliaji wa Yanga SC ya Tanzania ametwaa tuzo ya goli bora la mwaka katika CAF Awards 2025.

Mzize alifunga goli hilo Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe. Katika usiku wa tuzo zilizofanyika Morocco, Mzize aliwakilishwa na Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said.

Sababu kubwa ya mshambuliaji huyo kukwama kwenda kwenye usiku wa tuzo ni ushauri wa jopo la madaktari ambao walishauri asitembee umbali mrefu kutokana na upasuaji ambao amefanyiwa.

Hivyo tuzo ya goli bora CAF Awards 2025 imekuja nyumbani Tanzania.

Mbali na Mzize mchezaji Fiston Mayele ambaye aliwahi kucheza Yanga SC ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Mashindano ya Vilabu Barani Afrika (Men’s Interclub Player of the Year). 🇨🇩

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.