Yanga SC vs FAR Rabat CAF Champions League Novemba 22,2025 Dube nje ya msafara

Yanga SC vs FAR Rabat CAF Champions League Novemba 22,2025 maandalizi yanaendelea kwa wawakilishi wa Tanzania katika anga la kimataifa huku msafara unaotarajiwa kuelekea Zanzibar leo Novemba 18,2025 hautakuwa na mshambuliaji Prince Dube ambaye atakuwa nje ya msafara.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari Yanga SC, Ali Kamwe alibainisha kuwa msafara wa Yanga SC utaelekea Zanzibar leo kwa maandalizi ya mwisho mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FAR Rabat.

Timu itaondoka saa tatu asubuhi kwa njia ya boti huku baadhi ya wachezaji ikiwa ni Prince Dube, Celestine Ecua, Lassine Kouma waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa hawatakuwepo kwenye safari.

“Wachezaji ambao hawajarejea uongozi umefanya mpango maalumu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wataungana moja kwa moja na timu Zanzibar.

“Wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Tanzania wamesharejea na ni sehemu ya safari. Niwaombe Wazanzibar kujitokeza kwa wingi kuipokea timu na kuwaonyesha wachezaji wetu ni kwa kiasi gani mko tayari kwa ajili ya mchezo huu mkubwa wa Kihistoria. Zinakwenda kukutana timu mbili bora Afrika kwa sasa,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.