Simba SC vs Petro Luanda Novemba 23,2025, Camara out

Simba SC vs Petro Luanda mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Novemba 23,2025 ikiwa ni hatua ya makundi.

Mchezo huo awali ulipangwa kuchezwa Novemba 22,2025 saa 1:00 usiku lakini ratiba ilibadilishwa. Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally katika mchezo huo watamkosa kipa namba moja Moussa Camara ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United.

Ahmed amesema: “Kuhusu mchezo wa Ligi ya Mabingwa Aftika na tunathibitisha utachezwa Novemba 23, 2025 saa 10:00 jioni. Awali walipanga tucheze Novemba 22, 2025 saa 1:00 usiku lakini huo sio muda wetu mzuri wa mauaji hivyo tukafanya jitihada za kubadili muda.

“Mchezo wa Jumapili tutamkosa Moussa Camara ambaye yupo nchini Morocco alipokwenda kufanyiwa matibabu lakini pia tutamkosa beki wetu Abdulrazack Hamza ambaye na yeye anasafiri kwenda Morocco kwa matibabu zaidi. Taarifa njema ni kuwa Mohamed Bajaber amepona na hata mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania alianza na kucheza dakika 30,”.

Hii hapa bei ya viingilio

Viingilio vya mchezo ni Tanzanite – Tsh. 250,000, Platinum – Tsh. 150,000, VIP A – Tsh. 30,000, VIP B – Tsh. 20,000, VIP C – Tsh. 10,000 na Mzunguko – Tsh. 5,000.

Muda mfupi baada ya bei ya viingilio kutajwa Novemba 17,2025 taarifa kutoka Simba SC ilieleza kuwa Tanzanite tayari tiketi zimeisha.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.