Simba Yatangaza Viingilio vya Mechi Dhidi ya Petro Atletico ya Angola

Klabu ya Simba Sc imetangaza viingilio kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Petro Atletico ya Angola utakaopigwa Jumapili Novemba 23, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Meneja wa Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema Viingilio vya mchezo huo kwa tiketi za mzunguko ni Tsh 5,000, Tsh 10,000 kwa VIP C, Tsh 20,000 kwa VIP B na Tsh 30,000 kwa VIP A wakati tiketi za Platinum ni Tsh 150,000 wakati zile za Tanzanite zikiuzwa kwa Tsh 250,000