Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imepoteza mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kalenda ya FIFA kwa mabao 4-3 dhidi ya Kuwait, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Al Salaam, Cairo – Misri.
Tanzania ilianza vizuri mchezo huo na kupata bao la mapema dakika ya 7 kupitia Charles M’mombwa, kabla ya Allarakhia kuongeza la pili dakika ya 34. Hata hivyo, kipindi cha pili Kuwait ilirudi na nguvu na kusawazisha kisha kuongeza mabao kupitia Daham (46’, 52’), Naser (63’) na AlAnezi (69’).
M’mombwa alifunga bao la tatu kwa Taifa Stars dakika ya 87, lakini halikutosha kuokoa timu na mchezo kumalizika kwa ushindi wa Kuwait.
Matokeo ya mwisho:
Kuwait 4-3 Tanzania
Mabao ya Kuwait:
⚽ 46’ Daham
⚽ 52’ Daham
⚽ 63’ Naser
⚽ 69’ AlAnezi
Mabao ya Tanzania:
⚽ 07’ M’mombwa
⚽ 34’ Allarakhia
⚽ 87’ M’mombwa