Necta Yatangaza Mtihani Wa Kidato Cha Nne Kuanza Kesho – Wadanganyifu Watakiona Cha Moto


JUMLA ya watahiniwa 595,816 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) mwaka 2025, wakiwemo 569,914 wa shule na 25,902 wa kujitegemea.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Profesa Said Mohamed, amesema mtihani huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 17 hadi Desemba 5, 2025, na maandalizi yote muhimu yamekamilika ili kuhakikisha uendeshaji wenye uadilifu na usalama katika shule zote.