Pitso Mosimane ndani ya ardhi ya Tanzania kwa mradi wa Yanga Soccer School

PITSO Mosimane kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly amesema kuwa kuwafundisha watoto mpira ni jambo la lazima kwa kuwa huko ndiko wanatokea kuelekea katika timu za wakubwa.

Usiku wa kuamkia Novemba 15,2025 Pitso aliwasili Bongo akitokea Afrika Kusini ikiwa ni mualiko rasmi kutoka Klabu ya Yanga SC ambayo inatarajia kuzindua mradi wa Yanga Soccer School ili kukuza na kulinda vipaji vya watoto.

“Sio mara ya kwanza mimi kuwa hapa kwa ajili ya mualiko wa Yanga SC, niliwahi kuja wakati wa Wiki ya Mwananchi hivyo tumekuwa na urafiki mzuri na Yanga SC.

“Nimefurahi kuwa hapa na unajua kwamba ili kuwa na timu bora ni lazima kuwe na sehemu ambayo wachezaji wanatoka hivyo mradi huu wa Yanga School Soccer ninaona ni mzuri hata nchini Afrika Kusini nimekuwa nikifanya kazi kama hii,”.

Tukio la uzinduzi wa Yanga Soccer School linatarajiwa kufanyika leo Novemba 15,2025 Speedsports Muhimbili Center Dar ambapo Mosimane atakuwa mgeni rasmi na alipokewa na uongozi wa Yanga SC ukiongozwa na CEO Andre Mtine.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.