Timu ya Taifa ya Nigeria imetinga fainali ya mchujo wa awali wa kufuzu Kombe la Dunia Kanda ya Afrika (Play-Off Tournament) kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Gabon kwenye nusu fainali iliyopigwa katika dimba la Moulay El Hassan, Rabat Morocco.
Victor Osimhen alifunga magoli mawili kwenye mchezo huo uliolazimika kuamuliwa kwenye dakika 30 za ziada baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.
FT: Nigeria 🇳🇬 4-1 🇬🇦 Gabon ⚽️ 78’ Adams ⚽️ 97’ Ejuke ⚽️ 102’ Osimhen ⚽️ 110’ Osimhen ⚽️ 89’ Lamina Nigeria itachuana na mshindi wa mchezo nusu fainali nyingine kati ya Cameroon na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayoendelea hivi sasa.