Klabu ya Azam FC imemtangaza Octavi Anoro kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu kwa mkataba wa miaka miwili, hadi mwaka 2027. Anoro (42), raia wa Hispania, anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Abdulkarim Nurdin “Popat”, ambaye sasa amepandishwa cheo kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa klabu.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, Anoro anakuja na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika maendeleo ya utawala na biashara ya mpira wa miguu. Aidha, Bodi ya Azam FC pia imemteua Rashid Seif Mohamed kuwa Msaidizi wa Mtendaji Mkuu (Assistant CEO). Rashid ni mhitimu wa Shahada ya Umahiri ya Utawala wa Michezo (Master’s in Sports Management) na ana ngazi ya pili ya ukocha kutoka Chama cha Soka cha England, FA.