TIMU nne kutoka Tanzania zimetinga hatua ya makundi katika mashindano ya CAF ambapo mbili zipo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na mbili zipo katika hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba SC na Yanga SC zipo katika hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam FC na Singida Black Stars zipo katika hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi wa Tanzania, Singida BS na Azam FC wao wataanzia ugenini kutafuta ushindi.
Novemba 22, Singida Black Stars watakuwa nchini Algeria vs CR Belouizdad.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 4:00 usiku na kuruka mubashara kupitia AzamSports1HD.
Novemba 23, Azam FC watakuwa DR Congo Uwanja wa De Martyrs vs AS Maniema.
Mchezo huu utachezwa kuanzia saa 10:00 jioni na kuruka mbashara kupitia AzamSports4HD.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.