Azam FC hawataki utani wapya watano wanahitajika

MATAJIRI wa Dar, Azam FC hawataki utani msimu wa 2025/26 ambapo inatajwa kuwa katika dirisha dogo maboresho makubwa yatafanyika kwenye timu hiyo.

Mchezo uliopita Azam FC ilikuwa ugenini kwenye ligi na ubao ulisoma Namungo FC 1-1 Azam FC. Timu hiyo pia imetinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika hivyo ina kazi kubwa katika mechi za ushindani,

Taarifa zinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa Azam FC, Frolent Ibenge ameomba aboreshewe kikosi chake kwa kusajili wachezaji watano katika usajili wa dirisha dogo msimu huu,

Inaelezwa kuwa kocha amewaambia viongozi kuwa ili kikosi chake kifanye vizuri hatua ya makundi kuna umuhimu wa maboresho hayo.

Tetesi zinaeleza kuwa maeneo ambayo yatafanyiwa maboresho makubwa kwenye kikosi hicho ni ushambuliaji na kiungo ili kuwa bora zaidi kwa mechi zijazo.

Kwenye msimamo wa ligi Azam FC ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 5 baada ya mechi tatu ambazo ni dakika 270.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.