Yanga SC vs KMC FC, Uwanja wa KMC Complex Novemba 9,2025, Bacca, Mzize kukosekana

Yanga SC vs KMC FC ni mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex kwa miamba wawili kusaka pointi tatu muhimu.

Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye ligi tangu 2018 ni mara 14 wamekutana hivyo mchezo wa leo utakuwa ni wa 15 kwao katika msako wa pointi tatu muhimu.

Yanga SC alipata ushindi kwenye jumla ya mechi 11 huku KMC FC ikipata ushindi kwenye mchezo mmoja na sare ilikuwa katika mechi 2 pekee.

Wababe hawa Yanga SC vs KMC wanapokutana pointi husakwa kwa nguvu na magoli yanafungwa. Wananchi wamekuwa imara katika eneo la ushambuliaji huku wakusanya mapato wakiwa kwenye kasi ndogo.

Mara ya mwisho kwenye ligi wababe hawa walipokutana msimu wa 2024/25 ubao ulisoma KMC 1-6 Yanga SC kikiwa ni kipigo kikubwa kwa KMC FC kupokea kutoka kwa Yanga SC.

Edmund John nyota wa Yanga SC amesema wapo tayari kwa mchezo na wanahitaji pointi tatu muhimu katika mchezo wa leo.

Clement Mzize nyota wa Yanga SC hatakuwa kwenye mchezo wa leo kwa kuwa hayupo fiti na Ibrahim Bacca naye atakosekana kwa kuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 5.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.